Tuma mialiko inayopendeza kwa urahisi na faragha.
Mualiko hulinda faragha ya wageni wako na kufuta akaunti zao baada ya hafla yako.

Kwanini uchague Mualiko?
Gundua vipengele vinavyofanya Mualiko kuwa kivutio kwa wale wanaothamini urahisi wa matumizi na faragha.
Faragha
Hifadhi taarifa za wageni wako alizokuaminisha kwa faragha. Hakuna haja ya kuwapa mawakala.
Kadi zinazosarifika
Okoa gharama za kuchoresha kadi! Zisarifu kadi nzuri kuendana na hafla yako.
Mialiko inayohamishika
Tuma mialiko mingi kwa baadhi ya watu, na wao wanaweza kuzituma kwa wengine.
Kaimisha uhakiki
Wakaimishe unaowaamini kuwapokea na kuwahakiki wageni wako.
Matumizi bila mtandao
Hakiki wageni wako hata wanapokuwa hawana intaneti.
Ramani
Warahisishie wageni wako kufika eneo la hafla yako.

Utengezaji wa mialiko usio na tabu
Kupanga hafla yako haijawahi kuwa rahisi zaidi. Muonekano rafiki wa Mualiko kwa mtumiaji hukuruhusu kuunda kadi za mialiko kwa haraka. Iwe ni sherehe ya kuzaliwa, mkutano wa kampuni, au mkusanyiko wa kawaida, Mualiko hurahisisha mchakato wa mialiko kutoka mwanzo hadi mwisho.
Jaza maelezo ya hafla yako, sarifu kadi zako, na utume kwa wageni wako kupitia simu zao za mkonon. Ni rahisi sana! Mualiko app inashughulikia yote mengine. Pata urahisi wa kupanga hafla na Mualiko, na ushughulike na kile kinachojalisha - kujumuika na wageni wako.
Hakiki wangeni kwa usalama kwa kutumia tarakimu za kipekee
Mualiko inazingatia usalama na upekee wa hafla yako. Inahakikisha kwamba wageni waliyoalikwa tu ndio wanaweza kuingia kwa kutumia tarakimu za kipekee zilizowekwa ndani ya misimbo ya QR. Kila mualiko una tarakimu mahususi kwa kila mgeni ambazo ataonesha atakapofika hakuka hafla.

Jinsi inavyofanyakazi
Mualiko imesarifiwa kulinda taarifa za watumiaji wake na kuthamini faragha yao, pamoja na wageni wao.
Alika
Andaa kadi na upeleke mialiko kwa wageni wako.
Hakiki
Hakiki wageni kwa kuchanganua misimbo ya QR kwenye mialiko yao.
Futa
Akaunti zote za wageni wako na taarifa za hafla hujifuta baada ya tukio.
Bei zetu
Chagua kifurushi sahihi kulingana na mahitaji yako.
Angalia sampuli za kadi zetu
Sampuli mpya ya kadi huongezwa kila mara na zilizopo huboreshwa. Ona baadhi ya sampuli za kadi zilizo tayari kwa ajili ya hafla yako.

Pakua Mualiko
Mualiko unapatikana kwenye majukwaa yote maarufu: iOS 13+, Android 8+, na tovuti.

Waweza taka kujua
Una swali kuhusu Mualiko? Angalia majibu ya mausali ambayo tunahisi unaweza kuwa nayo. Ikiwa bado una masuali zaidi, tafadhali wasiliana nasi.
Mualiko ni programu ya usimamizi wa mialiko ya kidijitali inayowawezesha watumiaji kuunda, kutuma, na kudhibiti mialiko ya matukio kwa usalama na ufanisi.
Kwa sasa tuna offer ya uzinduzi inayokuruhusu kutengeza mialiko bila ya malipo. Wasiliana nasi kwa maelezo zaidi.
Unaweza kuandaa za mualiko hadi miezi 6 kabla hafla yako.
Ndio, unaweza kurekebisha mualiko wa hafla yako hadi saa 12 kabla ya kuanza.
Unaweza kuanza kuhakiki wageni wako saa 12 kabla ya muda wa hafla yako.
Ndio, wageni wote pia hupokea ujumbe mfupi katika simu zao wenye tarakimu za kipekee. Unaweza kuingiza tarakimu hizo wakati wa kuhakiki.
Ndio, Mualiko inakuwezesha kuwakaimisha watu wengine mchakato wa kuhakiki wageni, hivyo huna haja ya kusimama mlangoni mwenyewe.
Taarifa zote zinazohusiana na hafla pamoja na akaunti za wageni hujifuta masaa 12 baada ya muda wa kuanza hafla, kuhakikisha kwamba taarifa zako zinabaki faragha na salama.
Ikiwa utakutana na tatizo lolote, unaweza kuwasiliana na timu yetu ya msaada kupitia sehemu ya msaada au wasiliana nasi kupitia barua pepe kwa support@mualiko.com.